Wakitarajia kukipiga dhidi ya Polisi Tanzania kesho jumapili kikosi cha Singida Big Stars leo kimesepa kuelekea Karatu.

Mchezo huo wa ligi kuu unatarajiwa kupigwa kesho saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Black Rhino uliopo, karatu, Arusha.

Singida

 

Kikosi cha Singida Big Stars kiliondoka Singida mapema wiki hii kuweka kambi Arusha kujiandaa na mchezo huo ambao awali ulikuwa upigwe Jijini Arusha.

Singida Big Stars wanashuka kwenye mchezo huo wakiwa na pointi 14 baada ya kucheza mechi nane huku Polisi Tanzania wakiambulia pointi sita baada ya kucheza michezo 10 kwenye ligi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa