Singida Yatembelewa na Waziri Kambini Misri

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro na Rais wa TFF Wallace Karia wametembelea Kambi ya Timu ya Singida Fountain Gate iliyopo Cairo Misri ikijiandaa na mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Timu ya Future utakaochezwa Oktoba 1, 2023 Cairo nchini Misri.

Dkt. Ndumbaro ametembelea Kambi hiyo leo Septemba 28, 2023 baada ya kumaliza mkutano maalum wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) uliofanyika nchini humo jana Septemba 27, 2023.singidaAkizungumza na wachezaji hao amewaasa wacheze mpira wakiwa kwa kufuata maelekezo ya benchi la ufundi na kanuni za mpira ili kupata matokeo yatawapeleka hatua ya makundi.

“Tunawashukuru sana kwa kutuletea heshima nchi yetu na ninyi wenyewe, tusimwangushe Rais Samia Suluhu Hassani, sasa ni zamu ya Tanzania kwenye michezo, sasa ni zamu Singida Fountain Gate,” alisema Waziri Dkt. Ndumabaro.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Misri Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema furaha moja huongeza nyingine na amewatakia wachezaji hao ushindi mwema.

Naye Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Wallace Karia amesema Tanzania imekuwa na mwendelezo mzuri ambapo timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars imefika hatua nzuri ya kufuzu WAFCON na kupata fursa ya kuwa mwenyeji wa AFCON 2027 kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.singidaAidha, Rais wa Singida Fountain Gate Japhet Makau ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wa maandalizi ya Safari na mapokezi mazuri kutoka ubalozini Misri na kusisitiza kuwa Timu ipo salama na inaendelea na mazoezi kuelekea mchezo hu

Acha ujumbe