Skudu Yuko Fiti, Gamondi Aitahadharisha JKT TZ

Katika kuelekea mchezo wa raundi ya pili Ligi Kuu ya NBC, kati ya Yanga dhidi ya JKT Tanzania timu iliyopanda daraja msimu huu, Kocha wa Yanga Miguel Gamondi amesema kwamba kikosi kipo tayari kwa mchezo huo, huku akiweka bayana hali ya majeraha ya Winga Skudu Makudubela. Unaweza kubeti mchezo huu una odds kubwa Meridianbet.

“Licha ya kwamba mpinzani wetu tunajua ni timu iliyopanda daraja, najua kwamba wana wachezaji wenye uzoefu kwenye ligi hivyo hatupaswi kuichukulia kama timu dhaifu au ngeni kwenye ligi, ni wageni kwa maana ya timu lakini wana idadi kubwa ya wachezaji wenye uwezo lakini sisi ni timu kubwa na tupo nyuma nafikiri kesho tunapaswa kujiamini na kufunga magoli mengi”

Gamondi

“Kuna wachezaji kadhaa waliokumbwa na majeraha mchezo uliopita lakini kwa sasa wapo salama na tayari kuwavaa wapinzani wetu siku ya kesho na kuhusu Skudu ameshaanza mazoezi ya gym jana na wiki hii tutamweka kwenye uangalizi kisha baada ya hapo ataanza mazoezi na wachezaji wenzake”

Hata hivyo Gamondi amefafanua falsafa yake ya kucheza kwa kushambulia bila kujali anacheza na mpinzani gani, lengo ni kutoa burudani kwa wananchi. Odds kubwa unazipata Meridianbet pekee, bashiri na cheza kasino hapa.

CHEZA USHINDE

“Nina heshimu kila mpinzani ambaye tunakutana nae, falsafa yangu ni kucheza mchezo mzuri bila kujali tunacheza na nani, lengo letu kubwa ni matokeo pamoja na furaha kwa wananchi”-Miguel Gamondi kocha mkuu wa Yanga.

Mchezo huo utapigwa Jumanne Agosti 29/2023 katika dimba la Chamazi Complex majira ya saa 1:00 PM.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.