Tajiri wa Yanga Yusuf Manji Kuzikwa Leo.

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti na Mfadhili wa Yanga, Yusuf Manji ambaye alifariki juzi Jumamosi anatarajiwa kuzikwa leo nchini Marekani.  Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Manji alifariki akiwa hospitalini Florida Marekani alipokuwa anaishi kwa miaka mingi, na hata matibabu yake yalifanyika huku kabla ya umauti  kumfika.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo mtoto wa marehemu Mehbub Manji amelitumia Mwananchi inasema wao kama familia wanashukuru kwa jinsi ambavyo Watanzania wameendelea kuombeleza kifo cha baba yao na jinsi ambavyo wameendelea kumuombea huko alipo.

Kasino ya Mtandaoni usipange kuacha kucheza, Meridianbet wameakuandalia Maokoto na bonasi za kasino kibao.

“Tunawaomba muendelee kumuombea baba yetu awe na safari njema huko aendapo. Alikuwa anaipenda Tanzania na Watanzania wanampenda sana, lakini tunaomba kuwaambia kuwa Manji atazikwa leo saa tisa alasiri Orlando, Florida Marekani, karibu na sehemu aliyozikwa baba yake. Baba tulikupenda lakini Allah amekupenda zaidi. Yusuf Manji: Ni baba, rafiki, kiongozi,” ilimalizia taarifa hiyo.

MAMBAO 9 AMBAYO YUSUF MANJI ATAKUMBUKWA NAYO AKIWA YANGA.

(1) Yusuf Manji aliwai kuwalipia Viingilio Mashabiki wa Yanga Mechi ya Yanga na TP MAZEMBE, Mashabiki na Wanachama Wakaingia Bure.

(2) Manji Aliwalipia Viingilio Wanachama Wa Yanga kwa Ajili yakwenda Kuangalia Mechi ya Brazil na Taifa Stars, Brazil ya Akina Kaka.

(3) Manji alianzisha Week ya Wananchi na Kila Jumamosi kwa Miezi Miwili, Mashabiki na Wanachama wa Yanga Walikuwa Wakikutana Viwanja vya Mnazi Mmoja Wakila na kunywa gharama zote Zikibebwa na Yusufu Manji.

(4) Manji alishawahi kukodi Ma-Bus nakusafirisha Wanachama wa Yanga kutoka Dsm Kwenda Morogoro kuishangilia Yanga.

(5) Manji alishawahi kuwalipia Ada ya Uanachama Wanachama Wote wa Yanga kwa Mda wa Miaka Mitatu.

(6) Kipindi Hiko Jengo la Yanga likiwa Limechakaa zaidi, Manji aliweza kulifanyia Ukarabati nakulirudishiwa Muonekano Wakupendeza.

(7) Manji Aliwapa Yanga sehemu ya Ardhi ambayo Alikuwa anaimiliki Kigamboni ili Waweze Kujenga Uwanja Wao.

(8) Manji alikuwa na Vision kubwa sana na Yanga lakini Pia Yanga ilikuwa Moyoni mwa Manji.

(9) Manji ndiye Tajiri wa kwanza kupandisha Thamani ya Usajili na Mishahara kwa Wachezaji Nchini Tanzania.

Manji alisimama kama Kigezo na Kipimo Cha Mwekezaji yeyote Ndani ya Yanga na Simba

Kuna heshima yakipekee Yusufu Manji anastahili kwenye Soka letu.

Tajiri Manji alifariki akiwa anapatiwa matibabu nchini Marekani alipokuwa anaumwa kwa muda, Baada ya kuondoka Yanga Manji alibadilisha sehemu ya maisha yake yakawa New York Marekani.

Acha ujumbe