Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya Umri wa miaka 23, imeshindwa kuonesha makali yake dhidi ya Sudan Kusini jana kwenye uwanja wa Azam Complex- Chamazi, baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana.

Ni kama ndoto ya kijana ambaye amelala akaota yeye ni tajiri, lakini kuamka anajikuta yupo kwenye godoro jembamba mithiri ya ngozi ya ng’ombe, tena yupo kwenye chumba kidogo sana chenye mchanganyiko wa vyombo na kitanda.

 

Tanzania na Ndoto ya Kufuza AFCON

Naam, ni ndoto ya kufika Morocco Ardhi yenye vipaji vingi na miundombinu bora ya michezo, sio kwenda kutembea ni kwenda kuwaonesha kuwa Tanzania mpira upo, tuna kina Hackim, tuna wakina Mbappe, tuna kina Haaland wajao.

Tanzania imeanza safari kwa ugumu kiasi, hii itawafanya wahakikishe wanashinda mechi ya pili, ili kwenda kwenye hatua ya pili ya kufuzu mashindano ya AFCON chini ya miaka 23.

 

Tanzania na Ndoto ya Kufuza AFCON

Embu mtazame kidogo kijana aliyekulia ardhi ya mpira wa Tanzania pale Moro Town, kwa walima miwa mtibwa sugar, mtazame kidogo Alphone Msanga, tupa jicho kwa Novatus Dismas halafu rudi kwa fahari ya Tanga Abdul Suleiman Sopu, njoo tena kwa Kelvin John Mbappe, sijamsahahu The wonder kid Denis Nkane.

 

Tanzania na Ndoto ya Kufuza AFCON

Nataka kuamka lakini macho yanakataa kufunguka yana nambia umemsahahu kijana mwenye uwezo wa kutulia na mpira na kushambuliaji kwa kasi, tena ana movement tamu kama Ice Cream, Naam ni Tepsi Evance, baada ya kuwakumbuka majina haya ni kama nuru ya kufuzu AFCON nchini Morocco inaanza kumuliko kwenye macho ya Watanzania wengi. Bado haijaisha mpaka Iishe.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa