Klabu ya Tanzania Prisons imetangaza hii leo kuachana na aliyekuwa kocha wao Abdallah Mohamed Juma Barres.

 

Tanzania Prisons Yaachana na Kocha Wao

Kocha huyo alijiunga na klabu hiyo mwezi wa pili tarehe 1 kw amkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Prisons na hivyo klabu imeona ni muda sahihi wa kuachana na kocha huyo.


Taarifa hiyo ya kuachana na kocha Barres imetoka katika ukurasa wao wa Instagrama na Twitter na hivyo uongozi wa klabu hiyo unamtakia kila lakheri katika majukumu yake mapya nje ya timu yao.

Tanzania Prisons Yaachana na Kocha Wao

Tanzania Prisons imefanikiwa kubaki ligi kuu msimu huu, kwa kushika nafasi ya 8 baada ya michezo yake 30 na kukusanya poiti zake 37 sawa na Geita Gold ambaye alikuwa nafasi ya 7.

Msimu jana klabu hiyo ambayo makazi yake yapo Mbeya ilinusurika kushuka daraja baada ya kuponea kwenye play off na sasa hivi wamesema kuwa malengo yao ni makubwa na watapambana kwa kila hali na mali.

 


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa