Ligi kuu ya Tanzania Bara imeendelea hii leo na moja kati ya mchezo ulikuwa ni wa Tanzania Prisons kwa jina jingine (Wajelajela) dhidi ya Polisi Tanzania(Maafande) majira ya saa 8:00 mchana ambapo Polisi wameshindwa kupata alama hata.

 

Tanzania Prisons Yaimaliza Polisi Tanzania Hii Leo kwa 2-0.

Tanzania Prisons wakiwa wenyeji wa mchezo huo wamejikusanyia pointi tatu muhimu kwa kuicharaza Polisi mabao mawili kwa bila, huku mabao hayo yakifungwa katika dakika 45 za mchezo.

Bao la kwanza kwa Prisons lilifungwa katika dakika ya nne ya mchezo na Jeremiah Juma kwa mkwaju wa penati, na baadae katika dakika ya 45 ya kumalizika kwa  kipindi cha kwanza Samson Bangula anaipachikia bao Wajelajela na hatimaye mchezo kuisha kwa 2-0.

Tanzania Prisons Yaimaliza Polisi Tanzania Hii Leo kwa 2-0.

Ushindi huo walijipatia leo umewafanya wapande hadi nafasi ya 6 kwenye msimamo wa Ligi kuu ya NBC baada ya michezo yake 8 aliyocheza, huku kwa upande kwa Polisi Tanzania hali yake imezidi kuzorota kwani ameshuka hadi nafasi ya mwisho ya 16.

Polisi ndani ya  michezo 9 ameshinda mmoja peke yake huku wakiwa na kibarua kizito cha kujitafakari kabla mambo hayajaanza kwenda mrama na msimu kuisha kwani biashara ni asubuhi, mahesabu jioni.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa