SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza kufungua rasmi dirisha dogo la usajili kwa ajili ya vilabu vya ligi kuu, ligi daraja ya kwanza, na ligi kuu ya wanawake, ili kuboresha baadhi ya maeneo kwenye vikosi vyao.

 


Taarifa kutoka TFF ilieleza kuwa kuanzia leo Disemba 16 dirisha la usajili limefunguliwa na litafungwa Januari 15, hivyo vilabu vyote vinapaswa kukamilisha sajili za wachezaji wao ndani ya muda.

Iliendelea zaidi na kutanabaisha kuwa endapo timu yeyote itakutana na changamoto yeyote kwenye mfumo wa kuwasajili wachezaji wao TFF ipo tayari kutoa ushirikiano ili kukamilisha kila kitu.

Hapo awali tetesi za baadhi ya wachezaji kwenye dirisha la usajili kuhusishwa na vilabu vikubwa kama vya Simba SC, Yanga SC, Azam FC pamoja na timu zingine kutoka nje.

Majina yanayohusishwa sana kwenye Tetesi za usajili

Saidoo Ntibazonkiza

Mshambuliaji wa klabu ya Geita ambaye kwa sasa ameomba kuondoka klabuni hapo baada ya mkataba wake wa miezi 6 kukubaliana pande zote mbili.

 

dirisha la usajili

Kwa sasa anahusishwa zaidi na miamba ya kariakoo mitaa ya Msimbazi, Simba SC ambao wanahitaji kuimalisha zaidi safu yao ya ushambuliaji kuelekea michuano ya klabu bingwa.

Caser Lobi Manzok

Ni jina ambalo lilitawala sana tangu dirisha kubwa la usajili haswa kwa watani wa jadi Simba na Yanga, lakini mpaka dirisha la usajili linafungwa hakuna aliyeinasa saini ya mshambuliaji hatari aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Vipers United.

 

dirisha la usajili

Luis Jose Miquissone

Kijana aliyejizolea umaarufu mkubwa Tanzania haswa pale mitaa ya Msimbazi kwa mashabiki wa timu ya Simba SC, kuhusu kiwango chake hakuna hata mmoja anayepinga, ndio maana AL ahly ya Misri wakamsajili kwa pesa nyingi sana.

 

dirisha la usajili

Dirisha la usajili hili dogo jina lake limeendelea kusambaa zaidi kuhitajika na waajiri wake wa zamani Simba SC ambao kijana huyu wa Msumbiji alijiunga na miamba hao msimu wa 2018/2019 na kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi, FA, Mapinduzi, na Ngao ya Jamii na kuifikisha timu hayo hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ya Afrika CAFCL.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa