Katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam, timu zinazoshiriki ligi kuu ya NBC zimeng’ara baada ya kushinda mechi zao na kusonga mbele kwenye hatua inayofuata ya michuano hii.
Timu hizo zinatarajia kucheza hatua ya 32 ambapo kila mmoja akihitaji kufanya vizuri ili waweze kusonga mbele na kuchukua kombe hilo ikiwezekana ambapo zile timu zinazoshiriki ligi daraja la pili kwanza na tatu hali ikiwa mbaya.
Timu za Yanga, Simba, Azam, Tanzania Prisons na Ihefu ndio ambao wameweza kupachika mabao mengi hadi sasa kuanzia 8 kuendelea na ni wachezaji watatu tu ambao wameweza kutupia hat-trick.
Katika klabu ya Yanga ambao ndio mabingwa watetezi hat-trick ilifungwa na Clement Mzize, wakati kwa upande wa Simba ilifungwa na Mosses Phiri, Ismail Mgunda, halafu ikamaliziwa na Ihefu kupitia kwa mchezaji wao Andrew Simchimba.