TIMU ZATAKIWA KUCHANGAMKA NA KUJIIMARISHA

WAKATI wa sasa kwenye mashindano ambayo yanaendelea ni muhimu kila timu kukamilisha mipango iliyopanga kuikamilisha ndani ya mwaka.

Hakuna ambaye anapenda kuona kwamba anafungua ukurasa mpya wa mwaka huku mipango mingi ikiwa haijanikiwa kufikia pale ambapo ilikuwa inahitajika.TIMUIpo wazi kwamba kila mmoja ni lazima awe makini kwenye kutimiza majukumu yake kwa wakati uliopo na inawezekana kwa wakati ujao kufanya vizuri zaidi.
Muda haujawahi kutosha siku zote lakini kuna muda wa kufanya yale yaliyo ya umuhimu ili kukamilisha kile ambacho kipo kwenye malengo husika.

Timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara, Championship mpaka Ligi ya Wanawake ni muhimu kufungua ukurasa mpya wa hesabu kwenye wakati mwingine ujao.

Liishalo ni dogo kuliko lile linalokuja, kila hatua ina utofauti wake na kutimiza ni lazima kila mmoja kujitoa kweli katika kukamilisha hayo.

 

Iwe hivyo kwenye uwekezaji kwa wachezaji ambao wanasajiliwa pamoja na mashabiki ambao wanajitokeza uwanjani ni muhimu kuwa na maono mapya yatakayoongeza tija kwa timu kupata matokeo mazuri.

Malalamiko bila kutafuta suluhisho yatabaki kuwa hapohapo kwenye mpango kazi husika hivyo ni muhmu kila mmoja kufanya kwa umakini kutimiza mipango na inawezekana.TIMUMuda ni sasa kuangalia pale ambapo palikuwa na makosa na kufanyia kazi kwa umakini. Ikiwa itakuwa ngumu kurekebesha basi tusitarajie matokeo makubwa kesho.

Acha ujumbe