TRA United Yapania Kufufua Ndoto za Top Four Dhidi ya Coastal Union

Kocha wa Coastal Union, Fikiri Elias, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya TRA United utakaochezwa Juni 24, 2026, akieleza kuwa timu yake imejipanga kuonesha soka la kuvutia na kuondoka na matokeo chanya katika mchezo huo muhimu.

TRA United Yapania Kufufua Ndoto za Top Four Dhidi ya Coastal UnionTumejiandaa kupeleka ushindani na kuonesha burudani ya soka. Maandalizi yamekamilika vizuri na wachezaji wamezoea hali ya hewa ya Arusha, jambo linalotupa matumaini ya kupata alama tatu, alisema Fikiri wakati wa kuelezea maandalizi ya kikosi chake.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa upande wa wachezaji, Luician Kilua amesema morali ndani ya kikosi cha Coastal Union ipo juu huku kila mchezaji akiwa na hamu ya kupambana kwa nguvu zote ili kuhakikisha timu inapata ushindi muhimu katika hatua hizi za mwisho za msimu.

TRA United Yapania Kufufua Ndoto za Top Four Dhidi ya Coastal UnionNaye Kocha wa TRA United, Etienne Ndayiragije, amesema kikosi chake kipo tayari kwa pambano hilo baada ya kukamilisha maandalizi yake, huku akifurahishwa na kurejea kwa baadhi ya wachezaji waliokuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha. Timu ipo katika hali nzuri na kurejea kwa wachezaji wetu waliokuwa majeruhi kumeongeza nguvu na chaguo ndani ya kikosi, alisema Etienne.

TRA United Yapania Kufufua Ndoto za Top Four Dhidi ya Coastal UnionMchezaji wa TRA United, Ramadhan Salum ‘Chobwedo’, amesema timu hiyo inatarajia kutumia vyema faida ya kucheza nyumbani ili kupata ushindi utakaoweka hai matumaini yao ya kumaliza msimu katika nafasi nne za juu za msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.