Twiga Stars Kuanza Kampeni ya WAFCON 2026 Kwa Kukipiga dhidi ya Afrika Kusini

Timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, leo Julai 27, 2026, inaanza rasmi kampeni yake katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON 2026) kwa mchezo mgumu dhidi ya mabingwa watetezi, Afrika Kusini.

Twiga Stars Kuanza Kampeni ya WAFCON 2026 Kwa Kukipiga dhidi ya Afrika KusiniMchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Moulay Rachid uliopo Casablanca, Morocco, kuanzia saa 2:00 usiku, huku ukiwa mtihani wa kwanza kwa Twiga Stars katika harakati za kutafuta nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Twiga Stars ipo Kundi B pamoja na Afrika Kusini, Burkina Faso na Ivory Coast, kundi linaloonekana kuwa miongoni mwa makundi yenye ushindani mkubwa kutokana na ubora wa timu zilizopo.

Twiga Stars Kuanza Kampeni ya WAFCON 2026 Kwa Kukipiga dhidi ya Afrika KusiniKocha Mkuu wa Twiga Stars, Bakari Shime, amesema maandalizi ya kikosi chake yamekamilika na wachezaji wako tayari kupambana kwa nguvu zote ili kuanza mashindano hayo kwa matokeo mazuri dhidi ya mabingwa watetezi.

“Tumejiandaa vizuri kwa mchezo huu na tunaamini wachezaji wetu wako tayari kupambana. Tunaiheshimu Afrika Kusini, lakini tumejipanga kuhakikisha tunaanza WAFCON kwa matokeo chanya,” amesema Bakari Shime.

Twiga Stars Kuanza Kampeni ya WAFCON 2026 Kwa Kukipiga dhidi ya Afrika KusiniTwiga Stars itakuwa ikitafuta mwanzo mzuri wa kampeni yake ya WAFCON 2026, huku Watanzania wakisubiri kuona kama kikosi hicho kitaweza kuibua matokeo makubwa dhidi ya Afrika Kusini na kuongeza matumaini ya kufuzu hatua ya mtoano.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.