TIMU ya Taifa ya Tanzania Ya Wanawake (Twiga Stars) itashuka dimbani leo Ijumaa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi kucheza na Timu ya Taifa ya Afrika Kusini (Banyana Banyana).
Mchezo huo utakuwa ni wa kusaka tiketi ya kufuzu Mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika nchini Ufaransa baadae mwaka huu.
Kocha wa Twiga Stars Bakari Shime amesema, KIKOSI Chake kipo tayari na mchezo huo na Watanzania watarajie furaha