CHAMA cha soka wilaya ya Ubungo (UFA) kimesema kuwa kwa sasa kinaendelea na mashindano ya Ligi daraja la tatu na yanaendelea vizuri na wachezaji kwa ujumla wanaonesha hali na morali kwa ajili ya kupambania timu zao.

Akizungumzia hilo, Ofisa Tawala wa UFA, Benjamin Nungu amesema: “Ligi inaendelea vizuri, na wachezaji wote Wana hali na morali ya kupambana na wameonyesha Nia ya kupambana kwenye mashindano haya na yamekuwa na ushindani mkubwa sana.

UFA Cup

 

“Michezo ambayo imechezwa ni Urafiki planets wakishinda mabao 4 -2 dhidi ya mtambani FC, Kibamba utd dhidi ya Barney wao walitoka Suluhu bila ya kufunga na, huku Matosa Yanga Stars wakiibuka na bao 1-0 dhidi ya Tigers fc.

“Mashabiki tunawashukuru kwa sapoti zao waendelee kuja kuangalia burudani ya kutosha kwa vijana wao ili kuweza kuwasapoti na kikubwa tuweze kuwa pamoja na kutimiza malengo yetu ambayo tumejiwekea”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa