UKWELI KUHUSU SALIM TRY AGAIN NDANI YA SIMBA

JANA ilikuwa ni siku ya habari kubwa ambayo ilikuwa inahusu klabu ya Simba hasa kwa Wajumbe wa Kamati Tendaji ya klabu hiyo kuandika barua za kujiuzulu wadhifa hao moja wao akuhusishwa mwenyekiti Salim Try Again.

Ingawa mpaka Sasa Wajumbe wa Kamati hiyo upande wa Mwekezaji Mohamed Mo ambao wamethibitisha kutema bungo ni Hamza Johari na Rashid Shangazi.salim try againHuku taarifa za kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Simba zikisema wajumbe wote wa bodi ya wakurugenzi kutoka upande wa Mo wamejiuzuru huku sababu ikiwa ni presha kutoka Kwa tajiri Baada ya maendelezo wa vilio kwenye timu hiyo juu ya matokeo mabovu.

Pia taarifa zinadai kuwa hadi Mwenyekiti wa Bodi hiyo Salim Try Again amejiuzulu. Hali iyofanya Meridian Sports kuingia ndani na kuchimba ukweli wa taarifa hiyo.

Baada ya kumwaga jasho jingi kwenye kuchimba ukweli wa Try Again kuachia kiti. Meridian Sports limethibitisha kutoka Kwa mmoja wa watu wa karibu wa Try Again kuwa kiongozi huyo bado yupo yupo sana.salim try againHuku akisema Mo ana Imani kubwa sana Kwa Salim Try Again na haoni kama Kuna Sababu ya kumuondoa Kwa Sasa Kwa kuwa wamefanya mengi makubwa kwenye timu hiyo wakiwa pamoja.

“Try Again hajaandika barua ya kujiuzulu Simba na hakuna kitu kama hicho, yeye na Mwekezaji Wana mipango mikubwa ya kuijenga Simba mpya ya msimu ujao,” alisema mtoa taarifa huyo.

Acha ujumbe