VIONGOZI SIMBA WATOA KAULI YA KIBABE

SALIM Abdallah ‘Try Again’ ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba amewaambia mashabiki wa Simba kuwa wajiandae kufurahia msimu ujao kwa kuanzia ‘Simba Day’ huku akitamba kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu Bara wakiwa wamebakisha michezo mitano mkononi.

Kauli hiyo aliitoa wakati wakiwa katika maandalizi ya Tamasha la Simba Day litakalofanyika Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.SIMBAAbdallah aliongeza kuwa burudani hiyo wataipata kutoka kwa wachezaji wao wapya ambao wamewasajili baadhi ni Willy Onana, Fabrice Ngoma, Aubin Kramo na Fondoh Che Malone.

Aliongeza kuwa msimu ujao wamepanga kufanya vema na kikubwa ni kuhakikisha wanautangaza ubingwa mapema kabla ligi haijamalizika ya msimu ujao.

“Kwa usajili huu ambao Simba tumeufanya, basi naamini msimu ujao tutabeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara kabla ya mechi tano za mwisho, yaani tukiwa na mechi tano mkononi.

“Usajili wetu tuliofanya umeendana na mahitaji na mapendekezo ya kocha ambayo ameyafanya kwa kuwasajili wachezaji aliowahitaji.

“Hivyo mashabiki wa Simba wajiandae kufurahi msimu ujao, kwa kuanzia siku ya Simba Day Jumapili hii na kuendelea hadi katika Ngao ya Jamii,” alisema Abdallah.

Aliongeza kuwa msimu ujao wamepanga kufanya vema na kikubwa ni kuhakikisha wanautangaza ubingwa mapema kabla ligi haijamalizika ya msimu ujao.

“Kwa usajili huu ambao Simba tumeufanya, basi naamini msimu ujao tutabeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara kabla ya mechi tano za mwisho, yaani tukiwa na mechi tano mkononi.SIMBA“Usajili wetu tuliofanya umeendana na mahitaji na mapendekezo ya kocha ambayo ameyafanya kwa kuwasajili wachezaji aliowahitaji.

“Hivyo mashabiki wa Simba wajiandae kufurahi msimu ujao, kwa kuanzia siku ya Simba Day Jumapili hii na kuendelea hadi katika Ngao ya Jamii,” alisema Abdallah.

Acha ujumbe