Wakili wa mchezaji wa Yanga Feisal Salum Salum Nduruma amesema amepokea kwa masikitiko makubwa hukumu iliyotolewa na shirikisho la soka Tanzania kwa mchezaji wake.
Wakili wa mchezaji huyo anayefahamika kama Salum Ndruma Majembe anasema kua hukumu iliyotolewa na shirikisho na kumtaka Feisal Salum kurejea kwa klabu yake ya Yanga haijasimamia haki na wao wanaona mteja wao ameonewa.Feisal Salum aliitwa na shirikisho la soka Tanzania kamati ya sheria na hadhi za wachezaji juu ya shauri lake la kuvunja mkataba na klabu yake ya Yanga wiki kadhaa zilizopita, Na hukumu iliyotoka ilimtaka mchezaji huyo kusalia ndani ya klabu ya Yanga kwakua hakufuata taratibu katika kuvunja mkataba huo.
Wakili Salum Nduruma amesema watasubiri mpaka jumatatu kusikiliza ufafanuzi wa shirikisho hili ambapo maamuzi yakiwa hayohayo wataelekea mamlaka kubwa inahusiana na usuluhishi wa masuala ya kimichezo inayojulikana kama CAS.Taarifa kutoka ndani zinaeleza kua licha ya shirikisho kuamuru mchezaji Feisal Salum kurejea ndani ya klabu ya Yanga, Lakini mchezaji huyo hana mpango wa kuichezea tena klabu ya soka ya Yanga kutokana na namna ambavyo uongozi wa klabu hiyo umemtendea.