WATANO SIMBA KIKAANGONI

Wachezaji watano wa Simba Sc akiwemo Henock Inonga na Clatous Chota Chama wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi yao baada ya kufungwa na Yanga SC mabao 5-1 siku ya Jumapili.

Wachezaji hao wanatuhumiwa kuihujumu timu kitendo kilichopelekea kupoteza kwa idadi kubwa ya mabaoSIMBAMaamuzi hayo yamefanyika katika kikao cha bodi ya Wakurugenzi ya Simba kilichofanyika jana jijini Dar es salaam

Chanzo cha uhakika kutoka Simba SC kimeiambia Kishamba Media kuwa uongozi umeshapata ushahidi wa awali kuhusu tuhuma dhidi ya wachezaji hao na sasa imeanza uchunguzi wa kina ili kujiridhisha

Wachezaji hao watakua nje ya kambi ya timu mpaka hapo maamuzi mengine yatakapofanyika.SIMBAChanzo hicho kimesema huwenda leo klabu ya Simba ikatoa taarifa ya wazi kwa Umma juu ya maamuzi waliyofikia kuhusu wachezaji hao au wasitoe ila wahusika wamepewa taarifa

Maamuzi mengine yaliyofikiwa na bodi ni kufutwa kazi kwa kocha mkuu Robertinho, msaidizi wake pamoja na kocha wa viungo.

Acha ujumbe