INAAMINIKA na ipo wazi John Bocco kuwa ndiye mshambuliaji mzawa bora kwenye Ligi Kuu Bara Kwa takribani miaka 10 mfululizo akifunga zaidi ya mabao 100, Huku Wazir Junior akijaribu kufukuzia rekodi hiyo kwa karibu.
Bocco ameweka rekodi hiyo akiwa amezitumikia timu mbili tu, Azam FC na Simba SC zote za Dar Es Salaam.
Sasa Baada ya Bocco kumaliza yake, Kuna jina jipya limeibuka Msimu huu naye ni Wazir Junior King Of CCM Kirumba, ambaye msimu huu amekuwa wa moto sana kwenye kufunga.
Mpaka Sasa akiwa na Uzi wa KMC, Waziri ameshaingia kambani mara 11 na kuwa kwenye tatu Bora ya vinara wa mabao Ligi Kuu.
Lakini anaonekana kama anakwenda kuvaa viatu vya Bocco, kwani hadi Sasa akiwa amezitumikia klabu za Toto Afrika, Mbao FC, Biashara United, Dodoma Jiji, Yanga na KMC ameshafunga zaidi ya mabao 50.
Ambapo kwenye Ligi Kuu tu tayari ana mabao 50, achilia mbali vyuma ambavyo ameshaviweka kwenye FA na Mashindano mengine.
Junior amefikisha jumla ya mabao 50 aliyofunga kwenye Ligi Kuu tangu aanze kucheza soka la kulipwa.
Junior amefunga mabao huku akiwa amecheza jumla ya mechi 77 kwenye Ligi Kuu tangu akiwa na Toto Afrika ya Mwanza.
Takwimu zake
Toto Afrika- Mechi 13 na mabao 7 (2015-2016)
Toto Afrika- Mechi 17 na mabao 7 (2016-2017)
Azam FC- Mechi 1 hakuna bao (2017-2018).Biashara United (loan 6 month)- Mechi 6 mabao 3 (2018-2019). Mbao FC- Mechi 17 mabao 13 (2019-2020). Yanga SC -Mechi 4 mabao 2 (2020-2021). Dodoma Jiji (6 month)- Mechi 7 mabao 4 (2021-2022) na Sasa ndani ya
KMC- Mechi 3 bao moja (2022-2023).
KMC – Mechi 17 mabao 11 (2023-24) na bado msimu unaendelea ana nafasi ya kufunga zaidi ya hayo ikiwa atapata nafasi a kuzitumia.
Kutoka kwa beki mchawi, guu kubwa, Marco Mzumbe.