Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Yanga raia wa Burkinafaso Yacouba Sogne ametimkia klabu ya Ihefu Fc ya mkoani Mbeya baada ya kumalizana na Yanga.
Mchezaji Yacouba Sogne ambaye amekua ndani ya klabu ya Yanga kwa msimu wa tatu huu ameamua kuachana na klabu hiyo na kuelekea klabu ya Ihefu. Mchezaji huyo ambaye ametoka kwenye majeraha siku za karibuni amepewa mkono wa kwahera na Wananchi.
Mshambuliaji huyo ambaye amekua akiandamwa na majeraha kwa muda mrefu sasa na kusababisha kutokupata nafasi ya kudumu ndani ya klabu ya Yanga, Baada ya kupona majeraha yake amemalizana na waajiri wake hao na kuamua kuelekea klabu ya Ihefu ambayo inaonekana kufanya vizuri kwasasa kwenye ligi ya NBC.
Yacouba Sogne anajiunga na klabu ya Ihefu ya mkoani Mbeya kwa mkataba wa kudumu na sio kwa mkopo kama ambavyo taarifa zilieleza mwanzo kua ataenda Ihefu kwa mkopo. Mchezaji huyo anategemewa kwenda kufanya mambo makubwa kwenye klabu ya Ihefu na kukiimarisha kikosi hicho kutokana na uwezo wake.
Klabu ya Yanga inaelezwa kuachana na mshambuliaji Yacouba Sogne baada ya kufanya usajili wa mshambuliaji kutoka Zambia Kennedy Musonda ambae inaonekana amekuja kuziba nafasi ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Burkinafaso.


