Baada ya kutoka kwenye kibarua kizito wikiendi iliyomalizika dhidi ya Simba klabu ya Yanga kesho tena oktoba 26 itashuka dimbani na vijana kutoka Kinondoni jijini Dar-es-salaam KMC katika mchezo utakaopigwa katika dimba la Benjamini Mkapa.yangaKlabu ya Yanga ambayo haijapoteza nichezo takkribani 43 katika ligi kuu Tanzania Bara chini ya mwalimu Nasserdine Nabi wanaonekana kua timu yenye ubora na tishio katika ligi hiyo lakini wanakwenda kucheza na KMC  ambao nao wamekua kwenye kiwango bora siku za karibuni.

KMC wanakwenda kucheza na Wananchi kesho wakiwa wamepishana kwa alama moja 13 huku Wananchi wakiwa na alama 14 wakiwa pungufu ya michezo mitatu kwa maana ya KMC wakiwa wamecheza michezo 8 huku Wananchi wakiwa wamecheza michezo 6.yangaKMC ambao wameshinda michezo miwili mfululizo dhidi ya Ruvu Shooting na Azam na kuwafanya kusogea hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu wakiwa nyuma ya Yanga.

Wananchi kesho wanadondoka uwanjani kutafuta alama tatu muhimu ili kumtoa mtani wake Simba kileleni ambao atacheza siku ya alhamisi dhidi ya Azam.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa