YANGA IMEWAACHA MBALI

Klabu ya Yanga imeendelea kusaini Mikataba minono ya udhamini, Baada ya hii leo kusaini kandarasi na kampuni ya kuuza na kusambaza Pikipiki za Hero.

Mkataba huo utakaodumu kwa kipindi cha miezi 18 wenye thamani ya Tsh milioni 300, umeanza kutumika leo na utamalizika mwishoni mwa mwaka 2025.YANGAKwa upande wake Mkuu wa Masoko kutoka Karimjee Group, Nada Vievi, amesema pikipiki hizo zitakuja na Bima kwa mteja pamoja na kofia mbili zenye nembo za YANGA.

Huku Kwa upande wa Eng.Hersi Said – Raisi wa klabu ya Yanga, ambaye alisaini mkataba huo alisema: “Mkataba huu utaruhusu kwa matawi yetu ya Klabu kupata posho kwenye mauzo ya pikipiki hizo. Kwahiyo kila tawi linapaswa kuhakikisha biashara hii inakuwa kwa kasi. Hivyo basi kila mwananchi pikipiki yako ya kununua ni Hero na pikipiki ya kutumia ni Hero.YANGA“Tuwahakikishie kampuni ya Hero kuwa sisi ni Klabu namba moja na tutahakikisha wao ni namba moja waendelee kubakia kuwa namba moja. Uwezo wa kuifanya Hero kuwa namba moja ni jukumu la kila Mwanachama wa Young Africans, hivyo kuanzia sasa bodaboda ni Hero.

Acha ujumbe