UONGOZI wa Yanga unatarajia kuchinja ng’ombe 20 kwa ajili ya kugawa supu kwa mashabiki wa timu hiyo kabla ya tamasha la Wiki ya Mwananchi, Agosti 4 mwaka huu. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.
Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Mwananchi ambapo ametaja matukio manne watakayoyafanya kabla ya tamasha hilo.
Kamwe amesema wanatarajia kuanza kwa kufanya usafi kwenye Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, siku ya Jumatano na Alhamisi watachangia damu kwa watu wenye uhitaji.
Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi zinakaribia kuanza, usije kupishana na gari la Mshahara.
“Tulikuwa kimya, leo sasa ndio tumezindua rasmi Wiki ya Mwananchi tamasha maalumu kwa ajili ya kutambulisha kikosi chetu cha msimu kwa kufanya matukio hayo muhimu,” amesema.
Pia amesema Ijumaa watafanya dua maalumu kwa ajili ya kuwaombea watu wote waliotangulia mbele za haki, kuiombea timu, wachezaji, viongozi na mashabiki.
“Siku ya Jumamosi kutakuwa na tukio kubwa ambalo litakuwa maalumu kwa ajili ya kurudisha nguvu za wanachama na mashabiki zetu tukianza na kukimbia na baadaye Jangwani kutakuwa na supu,” amesema.
“Kwa taarifa nilizonazo nimesikia ng’ombe 20 watachinjwa Wananchi tutakunywa supu tayari kwa ajili ya siku yenyewe ya Jumapili ambayo itakuwa ni sikukuu yetu ‘Wiki ya Mwananchi’.”
Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.