Klabu ya soka ya Yanga imeendeleza rekodi yake ya kuendelea kucheza michezo ya ligi kuu Tanzania Bara baada ya kupata ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Geita Gold.

Klabu hiyo ilipata bao la mapema kabisa baada ya kupata mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na winga hatari Bernard Morisson ndani ya kipindi cha kwanza. Na ndio bao pekee lilidumu mpaka mchezo huo unamalizika katika dimba la CCM Kirumba.yangaklabu ya Yanga imefikisha michezo 45 bila kufungwa katika ligi kuu Tanzania Bara baada ya kupata ushindi wa dhidi ya klabu ya Geita Gold katika dimba la CCM Kirumba. na kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC.

Katika mchezo huo pia umeibua mjadala kutokana na mkwaju wa penati ambao mwamuzi aliutenga na kuipatia Yanga bao ilikua sio halali kwani mchezaji wa Geita aliunawa nje ya Eneo la hatari.yangaLakini kocha Cedric Kaze bado ameendelea kulia na ratiba ya ligi ambayo amelalamika inawaumiza. Ni kutokana na kucheza michezo mingi ndani ya siku chache na kukosa muda wa kupumzika kuelekea mchezo wao wa kombe la shirikisho dhidi ya Club Africain kutoka Tunisia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa