Klabu ya Yanga inatarajiwa kusafiri hapo kesho majira ya 9:25 mchana kuelekea Tunisia kwaajili ya kucheza mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain ambapo mchezo huo utapigwa tarehe 9.
Msafara huo utajumuisha wachezaji 22, benchi la ufundi 10 na viongozi 9 wa klabu hiyo, huku wakiwa na matumaini ya kupata matokeo mazuri ambayo yatawawezesha kuvuka hatua hiyo na kwenda hatua ya makundi.
Kwenye mchezo wa kwanza ambao ulipigwa siku ya Jumatano tarehe 2 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Yanga alikuwa ni mwenyeji wa mchezo alilazimishwa sare ya bila kufungana na Africain.
Na sasa anaenda uugenini kutafuta pointi ambazo zitamfanya afike hatua ya makundi kitu ambacho anahitaji nguvu ya ziada kwani mechi ya hapa nyumbani hakuonyesha kile ambacho kilitakiwa aonyeshe.
Katika mechi hizi za mtoano inabidi unapopata nafasi uzitumie kwani badae huleta majuto kutokana na kushindwa kufanya kilichotakiwa. Yanga inabidi ionyeshe juhudi ya hali ya juu kwani Club Africain wanaweza kupata matokeo mbele yao.