YANGA KUMSHUSHA SOWAH

Kwa mujibu wa Chanzo Cha kuaminika kutoka nchini Ghana kimethibitisha kuwa Mshambuliaji Jonathan Sowah (25) ameshasaini Mkataba wa Mwaka Mmoja wakuitumikia Yanga.

Mkataba ambao una kipengele cha Kuongezewa mwaka mwingine au zaidi kama atawaka mapema.

Taarifa kutoka Ndani ya Yanga zimethibitisha kuwa Sowah anakuja kuvaa viatu vya Mshambuliaji Raia wa Ivory Coast Joseph Guede ambaye kandarasi yake imeisha na hakukuwa na Mazungumzo nae tena ya kumuongeza Mkataba Mpya baada ya ule wa Miezi 6 kutamatika.

Acha ujumbe