Uongozi wa Klabu ya Yanga umetenga kiasi cha zaidi ya milioni 500 Kwa wachezaji wa timu hiyo kama watashinda mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelody Sundowns.
Mmoja wa viongozi wa Klabu hiyo ameiambia Meridian Sports kuwa fedha hizo ni sehemu ya bonus na Kuna Uwezekano ikafika zaidi ya milioni 500 Kwa kuwa Kuna ahadi nyingine kutoka Kwa viongozi.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Kiongozi huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina Kwa kuwa siyo msemaji wa timu alisema: “Kuna bonus zaidi ya milioni 500 ipo mezani Kwa ajili ya wachezaji wetu, kama wakiwafunga Mamelody Sundowns.
“Huenda pia fedha hiyo ikaongezeka kutokana na ahadi ambazo zinazidi kuongezeka kutoka Kwa mashabiki wetu na baadhi ya viongozi waliopo nje ya timu.”
Kwa upande wa msemaji wa Klabu ya Yanga Ali Kamwe alisema: “Ushindi kwenye huu mchezo ni jambo la Lazima kwetu, tunahitaji kuionesha Afrika ubora wetu na Hilo linakwenda kutokea.”