YANGA KUTESEKA TENA KWA IHEFU

KESHO Jumatano, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Klabu ya Yanga, watashuka kwenye dimba ambalo waliteseka sana msimu uliopita, Highland Estate Mbeya, kucheza na Ihefu.

Msimu uliopita Yanga walifungwa mabao 2-1 na Ihefu na kuvunjiwa safari yao ya kutafuta Unbeaten 50 kwenye msimu jana. Kesho Yanga watakuwa na kazi ya kulipa kisasi ili waendelee kubaki kieleleni.YANGAKocha wa Ihefu Zubeir Katwila yeye amesema kuwa mateso yatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga, kwani hawatapata hata sare kwenye mchezo huo kwa kuwa mpango wao ni kuvuna alama tatu.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu ila tumejiandaa kucheza nao, msimu uliopita tulipata alama kwao na kesho pia tunataka alama tatu.YANGA“Mechi hii haina utofauti na kama nikicheza dhidi ya Kagera Sugar, Dodoma Jiji na timu nyingine labda utofauti ni tumekutana nao mzunguuko wa nne tofauti na msimu uliopita,” alisema Katwila.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.