YANGA NA CHIVAVIRO MAZUNGUMZO YANAENDELEA

INAELEZWA kuwa, mabosi wa Yanga wameanza mazungumzo rasmi na uongozi wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini juu ya uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo, Ranga Chivaviro katika usajili wa dirisha dogo.

Yanga imekuwa ikitafuta mbadala wa Fiston Mayele aliyetimkia Misri katika Klabu ya Pyramid ambapo nafasi yake ilizibwa na Hafiz Konkoni ambaye ameshindwa kuonyesha makali yake ndani ya kikosi hicho hali iliyopelekea kuweka nguvu ya kumpata Chivaviro.YANGALicha ya uongozi wa juu kuweka bayana kuwa suala la usajili ndani ya timu hiyo kwa sasa lipo chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi, inafahamika kuwa tayari mabosi wa timu hiyo wamekuwa na mawasiliano na viongozi wa Kaizer Chiefs juu ya uwezekano wa usajili wa mshambuliaji huyo.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo, kimesena kuwa kwa sasa wapo katika mazungumzo ya kuona wanalimaliza vipi suala la kumpata mshambuliaji huyo wa kati kutoka Afrika Kusini.

“Ni kweli tumekuwa na mazungumzo na viongozi wa timu ambayo anacheza huyo mchezaji kwa sababu bado nafasi ya mshambuliaji wa kati imekuwa tatizo na huyo mtu tunaona anaweza kutusaidia katika eneo ambalo tumeshindwa kupata dawa, kama kila kitu kikienda sawa basi tunategemea kuwa naye hapa,” alisema mtoa taarifa.

Kwa upande wa rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, alisema kuwa kwa sasa suala zima la usajili lipo chini ya kocha wa timu hiyo kwa kuwa ndiye anatambua wachezaji anaowataka kwenye kikosi chake.YANGADesemba 16, mwaka huu, usajili wa dirisha hapa nchini unatarajiwa kufunguliwa ambapo timu mbalimbali zitakuwa na nafasi ya kuimarisha vikosi vyao

Acha ujumbe