Yanga na Singida Big Stars Kuzichapa Leo

Klabu ya Yanga inatarajia kuwaalika Singida Big Stars hii leo katika uwanja wa Benjamin Mkapa kwaajili ya mchezo wao wa Ligi kuu ya Tanzania Bara unaotarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 usiku.

 

Yanga na Singida Big Stars Kuzichapa Leo

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya NBC msimu uliopita wamejipanga kuwakabili walima alizeti hao kutoka Singida baada ya kuvuna alama tatu mchezo uliopita wakiwa ugenini dhidi ya Kagera Sugar.

Vilevile Singida nao ambao wamepanda Ligi msimu huu, wameanza vizuri ligi baada ya kuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo na pia kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa na uzoefu wa Ligi wakiwemo Kagere, Wawa na wengine wengi.

Mechi yao iliyopita wametoka kutoa sare na Wekundu wa Msimbazi baada ya kuanza kupachika bao dakika za mapema kabisa kabla ya bao hilo kuja kusawazishwa na kuondoka na alama moja moja.

Yanga na Singida Big Stars Kuzichapa Leo

Yanga wao wakiwa hawajapoteza mchezo wowote mpaka sasa wamesema kuwa wamejiandaa vizuri kwa mechi hii ya leo, licha ya kuwa na ratiba ngumu na pia kucheza mechi za hapa na pale lakini watafanya juhudi kupata ushindi.

Singida nao wamesema wapo tayari kushuka dimbani kuzisaka alama 3 zitakazowasaidia kusogea mbele kutoka hadi nafasi waliyopo. Tofauti ya pointi kati yao ni pointi 5 huku walima alizeti wakiwa na mchezo mmoja mbele.

Acha ujumbe