YANGA NI KAZI JUU YA KAZI MOROCCO

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa mpango kazi mkubwa kwenye mechi yao dhidi ya Waarabu wa Algeria, CR Belouizdad.

Timu hiyo inakibarua cha kuanza kusaka ushindi kwenye mchezo wa hatua ya makundi Novemba 24 kisha wakimaliza kazi hiyo watarejea Dar kumenyana na Al Ahly Desemba 2.YANGAGamondi amesema kuwa kila mchezo ni muhimu kupata ushindani hasa kwenye mechi za kimataifa ambazo ushindani wake huwa mkubwa.

“Kila mchezo una umuhimu kwetu kushinda ipo hivyo na wachezaji wanatambua kwamba kipi ambacho tunahitaji katika kila mchezo ambao tunacheza iwe ni kitaifa ama kimataifa.
“Wapinzani tulionao sio wa kuwabeza, tunawatambua na tunawaheshimu hivyo ambacho tunahitaji ni kuwa kwenye mwendo mzuri na kupata matokeo kwenye mechi zetu ambazo tutacheza,” amesema Gamondi.

Tayari kikosi cha Yanga msafara wa kwanza umewasili Algeria kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo na msafara wa pili unatarajiwa kuwasili leo.
Ni wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya taifa ikiwa ni pamoja na Dickson Job, Bacca hawa walikuwa na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.YANGAKwenye msafara wa kwanza ni Zawad Mauya, Kibwana Shomari, Maxi Nzengeli hawa wapo na timu Algeria kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ijumaa

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.