Kocha Mkuu wa Yanga SC, Abdihamid Moalin, amesema kikosi chake kimekamilisha maandalizi ya mchezo wa kesho dhidi ya TRA United, akieleza kuwa licha ya kuwaheshimu wapinzani wao, lengo lao ni kuibuka na ushindi ili kuendelea na harakati za kutetea ubingwa.
“Tunawaheshimu TRA United, lakini tumejiandaa kushinda mchezo huu,” amesema Moalin. Naye mchezaji wa Yanga SC, Abuutwalib Msheri, amesema mchezo huo una umuhimu mkubwa kwa mabingwa hao watetezi, huku akiwataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kuisapoti Yanga SC uwanjani.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa upande wa TRA United, Kocha Mkuu Etienne Ndairagije amesema timu yake haikuingia msimu huu ikiwa na malengo ya kufuzu michuano ya kimataifa, bali ililenga kujijengea heshima na kuitambulisha vyema kwenye Ligi Kuu. “Hatukuwa na malengo ya Kimataifa, bali kuitambulisha timu kwenye Ligi Kuu na kuendeleza mwenendo wetu mzuri,” amesema Ndairagije.
Naye mchezaji wa TRA United, Shaaban Idd Chilunda, amesema michezo dhidi ya timu kubwa huwa na ushindani wa hali ya juu, jambo ambalo limewapa hamasa ya kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya kupambana na Yanga SC na kutafuta ushindi.
Yanga SC na TRA United zitakutana kesho, Juni 27, 2026, saa 10:00 jioni, katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku kila upande ukiwa na malengo tofauti lakini ukiwania alama tatu muhimu.


