KIKOSI cha Yanga SC kimeondoka mapema leo kuelekea Tunisia kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa mtoano wa michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Club Africain ya nchini humo.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Novemba 9 mwaka huu ambapo katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye dimba la Mkapa Jijini Dar Es Salaam, ulimalizika kwa sare ya kutokufungana.

 

Yanga SC Yatinga Tunisia Kibabe

 

Hivyo ili Yanga waweze kuvuka katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Shirikisho wanapaswa kushinda au kutoa sare ya magoli yeyote, ila mchezo kama utamalizika kwa sare ya kutokufungana itabidi mikwaju ya penati iamue nani anakuwa mshindi.

Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema “Tumeumizwa na matokeo yaliyopita ya suluhu na hakuna mtu yeyote ambaye amejiandaa nayo. Tunawaomba wana Yanga kuwa wamoja na kuisapoti timu yetu tunaamini bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye dakika 90 za mchezo wa marudiano kule Tunisia.

 

Yanga SC Yatinga Tunisia Kibabe

“Kwenye mpira lolote linawezekana tumefanya vibaya kwenye mchezo wa nyumbani kwa kutoka suluhu lakini tutaenda kupambana kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mchezo wa marudiano.”

Yanga SC walianzia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika na kutolewa, na AL-HILAL ya nchini Sudan.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa