Yanga SC, Leo jumanne ya OKtoba 31, imetembelewa na Balozi wa Uingereza David Concar, Ziara yenye mafanikio makubwa kwa lengo la kusisitiza uhusiano kati ya Uingereza na Tanzania katika sekta ya michezo kwa maendeleo makubwa katika soka la Tanzania.
Lakini kabla ya hapo Balozi Concar alikuwa ameitembelea klabu ya Simba, mapema leo asubuhi.Balozi David Concar amekutana na Rais wa Yanga SC, Eng. Hersi Said, Makamu wa Rais Arafat Haji, Afisa Mtendaji Mkuu Andre Mtine, Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe. Kocha Mkuu Miguel Gamondi pamoja na Nahodha Bakari Mwamnyeto.
Balozi wa Uingereza David Concar ametembelea mazoezi ya Yanga SC na kufanya mazungumzo na wachezaji huku akitoa moyo na kuwaunga mkono wachezaji wenye vipaji vya kucheza mpira wa miguu nchini Tanzania.
Yanga SC inaendelea na kujifua Avic Town kwa ajili ya mchezo wa watani wao wa jadi Simba SC.Mapema Leo Balozi David Concar aliitembelea Simba SC na kutazama mazoezi ya leo asubuhi ikiwa ni maandalizi ya mchezo wao wa jumapili dhidi ya Yanga SC