YANGA WAKUTANA KUJADILI YA MSIMU UJAO

Kamati ya Utendaji ya Yanga SC chini ya Rais Eng.Hersi Said jana tarehe 07/06/2024 ilifanya kikao maalumu cha maandalizi ya Mkutano mkuu wa Wanachama (Annual General Meeting – AGM).

Kikao ilichofanyika katika ukumbi wa Urban By City Blue, Masaki Jijini Dar Es Salaam. Huku malengo na ajenda Kuu ya kikao hicho ni mipango ya kwenda kuutikisa tena Msimu Ujao.yangaOfisa Habari wa Yanga Ali Kamwe alisema huo ni Utaratibu wa kawaida na wakikatiba ambao unawataka viongozi wa juu kukutana Baada ya Msimu kumalizika Ili kujadili mipango ya Msimu Ujao.yanga“Viongozi wa juu wa Klabu yetu walikutana na kufanya kikao, huku ajenda Kuu ikiwa ni Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Yanga na mipango ya kwenda kuutikisa tena Tanzania na Afrika Msimu Ujao, ” alisema KAMWE

Acha ujumbe