YANGA WANA KAZI NA KAGERA SUGAR

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi wanatarajiwa kumenyana na Kagera Sugar, Uwanja wa Mkapa.

Ipo wazi kuwa Yanga haijapoteza mchezo wowote msimu wa 2023/24 ikiwa nyumbani hivyo Kagera Sugar wanakazi kubwa kufanya ugenini.yangaKocha Mkuu wa Yanga, Miguel gamondi amebainisha kwamba wapo tayari kwa mchezo huo na kikubwa ni kuona kwamba wanapata pointi tatu muhimu.

“Tupo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu kwenye mchezo wetu.”

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Kaitaba baada ya dakika 90 ubao ulisoma, Kagera Sugar 0-0 Yanga.yangaPia Obrey Chirwa bao lake lilifutwa kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa katika mtego wa kuotea
Yanga ipo nafasi ya kwanza katika msimamo Ina pointi 65 inakutana na Kagera Sugar iliyo nafasi ya 7 na pointi 30 zote zimecheza mechi 25.

Acha ujumbe