Wapinzani wa Yanga kimataifa, CBE SA ya Ethiopia wameipa Yanga jumla ya milioni 35 kwa kufungwa jumla ya mabao 7-0 ndani ya dakika 180 katika anga la kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Rekodi imeandikwa Septemba 21 2024 Young Africans inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi kutinga hatua ya makundi kwa ushindi wa mabao 6-0 CBE SA katika mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex.
Mabao ya Young Africans yalifungwa na Clatous Chama dakika ya 35, Clement Mzize dakika ya 46, Aziz Ki dakika ya 74, 90, Mudathir Yahya dakika ya 88 na Duke Abuya dakika ya 90.
Yanga inatinga hatua ya makundi Ligi ga Mabingwa Afrika mara mbili mfululizo baada ya kufanya hivyo mara ya kwanza msimu wa 2023/24.




