Yanga watisha Kibabe Siku ya Wananchi

TAMASHA la kilele cha wiki ya Mwananchi kilichofanyika leo jumamosi kimefana kutokana na burudani mbalimbali ambazo zilifanyika kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Miongoni mwa burudani hizo ni wasanii mbalimbali ambao wametumbuiza pamoja na michezo iliyochezwa.

Utambulisho wa nyota wapya wa Yanga uliofanywa na Haji Manara umeonekana kuteka hisia za mashabiki wengi ambao wamejitokeza kwenye Uwanja wa Mkapa.
Licha ya mashabiki wa Yanga kufurahia utambulisho wa wachezaji wao lakini Stephane Aziz Ki ndiye mchezaji ambaye ameshangiliwa sana wakati wa utambulisho wake.
Mashabiki wamejitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Mkapa kwa ajili ya kushuhudia tamasha hilo kubwa ambalo limetumika kwa ajili ya utambulisho wa nyota wapya pamoja na wale wa mwanzo.

Acha ujumbe