KIKOSI Cha Yanga ambacho kipo Afrika Kusini kwenye maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Mamelodi Sundowns Imeanza kazi rasmi ya kusaka nafasi ya kwenda nusu fainali.
Ofisa Habari wa Yanga Ali Kamwe alizungumza na Meridian Sports kuhusiana na hali ya mambo yanavyoendelea wakiwa Sauz, alisema timu haijalala na imeshaanza kazi.“Naomba niwaambie mashabiki wa Yanga na wale wote wenye mapenzi ya dhati ya timu yetu. Kuwa Kazi Imeanza Kwa haraka sana hapa Sauz.
“Kilichotuleta hapa ni kitu kimoja tu, kusaka nafasi ya kusonga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.“Kazi Imeanza haraka hapa Pretoria na Wapinzani wetu wameshapata habari zetu juu ya kile tunachotaka kwako,” alisema Ali Kamwe.