Baada ya ushindi wa jana wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo, klabu ya Yanga imeanza safari ya kurejea Dar es salaam kupitia Mtwara wakitokea Ruangwa ambapo jana walikuwa na kibarua kizito huko Lindi.

 

Yanga Yaanza Safari Kutoka Lindi
Yanga wameendelea kusalia kileleni baada ya jana kuchana nyavu mara mbili kupitia kwa wachezaji wao Yanick Bangala na Tuisila Kisinda ambayo yalitosha kuikandamiza Namungo huku wakiwa wamezidiwa kwa ubora.

Pointi tatu za Yanga zimewafanya wawe mbele kwa pointi nne kileleni na kuwa na matumaini ya kutetea taji lao ambalo walilichukua msimu uliopita chini ya Nasredine Nabi japokuwa kocha huyo amefungiwa michezo mitatu na faini juu.

Yanga Yaanza Safari Kutoka Lindi

Kikosi hicho kinatarajiwa kushuka dimbani kwa Mkapa siku ya Jumapili kukipiga dhidi ya Kurugenzi FC kwenye mchezo wa Azam Sports Federation Cup ambapo wao ndio mabingwa watetezi wa Kombe hilo baada ya kumtwanga Coastal Union.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa