Yanga Yachapika Benjamin Mkapa

Ligi kuu ya NBC iliendelea hapo jana kwa mchezo mmoja ambao ulikuwa ukiwakutanisha kati ya Azam FC dhidi ya bingwa mtetezi Yanga majira ya saa 2:30 usiku.

Yanga Yachapika Benjamin Mkapa

Mchezo huo ulipigwa katika dimba la Benjamin Mkapa baada ya mwenyeji Azam kuomba kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) mchezo huo kupigwa katika uwanja huo ambao kwasasa unatumika kwenye mechi za ligi ya mabingwa pekee.

Yanga walianza kufunga bao kupitia kwa kiungo wao Aziz Ki kabla ya Jibril Silla kuja kusawazisha bao hilo na kwenda mapumziko mzani ukiwa unasoma bao moja kwa moja huku timu zote zikishambuliana haswa.

Baada ya kurejea uwanjani dakika ya 51 Feisal Salum akaipatia Azam bao la pili la kuongoza na ndilo ambalo lilisalia mpaka dakika zote 90 za mchezo na mchezo kuisha kwa 2-1 licha ya vijana wa Gamondi kufanya mashambulizi mengi ambayo hayakuzaa matunda.

Yanga Yachapika Benjamin Mkapa

Baada ya mechi kuisha Young Africans anasalia kileleni akiwa na pointi zake 52, akifuatiwa na Wanalamba lamba wakiwa na pointi zao 47 na Simba akiwa na pointi 45 na michezo mkononi hadi sasa.

Mchezo unaofuata kwa Yanga ni dhidi ya Mamelodi kwenye ligi ya mabingwa hatua ya robo fainali ambao utapigwa siku ya Jumamosi taraehe 30 mwezi huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

 

 

Acha ujumbe