Klabu ya Yanga imeshindwa kuchukua pointi 3 na kuchukua moja pekee kwenye mchezo wa jana huko Mali ambapo walikuwa wakimenyana dhidi ya Real Bamako.

 

Yanga Yachukua Pointi 1 Mali

Yanga walitangulia kupachika bao kupitia mshambuliaji wao hatari Fiston Mayele katika dakika ya 60 kwenye kipindi cha pili cha mchezo kabla ya Emile Kone kuja kusawazisha bao hilo dakika ya 90.


Baada ya sare hiyo vijana wa Nabi wanashikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na pointi nne huku kinara wa kundi hilo akiwa ni Monastri ambaye ana alama zake saba hadi sasa.

Yanga Yachukua Pointi 1 Mali

Huku nafasi ya mwisho ikishikiliwa na Real Bamako ambaye ana pointi mbili pekee kwenye michezo mitatu aliyocheza. ODDS KUBWA unazipata Meridianbet pekee ingia na ucheze.

Baada ya sare hiyo Wananchi watarejea nyumbani tena kukiwasha dhidi ya huyo huyo Bamako mchezo wa marudiano ambao utapigwa Machi 7.

 

 


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa