Klabu ya Yanga imeendelea kushika mkia katika kundi lake kwenye ligi ya mabingwa Afrika baada ya kutoka suluhu ya bao moja kwa moja dhidi ya Medeama ya nchini Ghana.
Yanga leo walikua ugenini nchini Ghana kumenyana na klabu ya Medeama na kujikuta wakiambulia sare ya bao moja kwa moja, Hivo klabu hiyo kuendelea kushika mkia kwenye kundi D.Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya NBC wamefanikiwa kukusanya alama mbili baada ya kucheza michezo mitatu, Hii inawapa wakati mgumu klabu hiyo lakini wanaweza kufanya makubwa kuelekea mchezo wao unaofuata.
Mchezo unaofata Wananchi watakua nyumbani jijini Dar-es-salaam kurudiana na Medeama, Mchezo huo unaweza kua wa matumaini kwa klabu hiyo kama watafanikiwa kushinda kwani watakua na alama tano na kuweza kufufua matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali.Klabu ya Yanga inashika mkia huku Al Ahly wakiwa kileleni kwa alama tano baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana wakiwa nyumbani na klabu ya CR Belouzdad, Lakini wakiwa na matumaini makubwa kutokana na michezo miwili ya nyumbani inayofuata dhidi ya Medeama na CR Belouzdad.