Klabu ya Yanga imesafiri leo hii kuifuata Geita Gold ambapo wanatarajia kucheza mchezo wao wa Ligi kuu ya NBC hapo kesho majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa CCM Kirumba.

 

Yanga Yaifuata Geita Gold Leo Hii.

Yanga ambayo ipo chini ya kocha mkuu Nasreddine Nabi mpaka sasa wametimiza michezo 44 bila kufungwa huku mchezo wa mwisho wakishinda kwa bao moja kwa bila dakika za jioni za mchezo huo.

Msimu huu amecheza michezo saba ya ligi na ndani ya michezo hiyo ameshinda mitano, ametoa sare mbili na hajapoteza mchezo wowote mpaka sasa, nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi huku akiwa na pointi 17.

Yanga Yaifuata Geita Gold Leo Hii.

Wakati kwa upande wa vijana wa Fred Minziro wao msimu huu wamejivunia pointi 13 baada ya kucheza michezo 9, wameshinda michezo mitatu, wameenda sare mara nne na wamepoteza michezo miwili.

Ikumbukwe kuwa Geita Gold walipanda daraja msimu jana ambapo mechi zote mbili alizokutana na Yanga alipoteza kwa jumla ya mabao 2-0, huku aliyekuwa mchezaji wao Saido Ntibanzokiza akihamia kwa wachimba madini na kuendeleza kiwango chake bora alichoondoka nacho.

Yanga Yaifuata Geita Gold Leo Hii.

Kwahiyo hautakuwa mchezo mwepesi kwani kila timu itacheza kuhitaji pointi tatu muhimu hasa kwa Young Africans ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi watahitaji kutetea taji hilo tena.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa