Baada ya kupata ushindi mwembamba hapo jana wa ligi, klabu ya Yanga imeifuata Real Bamako ya nchini Mali kwaajili ya mchezo wao wa tatu kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Yanga ambayo ipo chini ya kocha mkuu Nasredine Nabi walishinda mchezo wao wa pili dhidi ya TP Mazembe wakiwa kwa Mkapa kwa mabao 3-1 na kujikusanyia pointi tatu huku wakishika nafasi ya pili.
Real Bamako yeye ndiye kibonde wa Kundi hilo D akiwa hajashinda mchezo wowote lakini ametoa sare mchezo mmoja, hivyo mechi yake hiyo inayofuata ya nyumbani anatarajia kupata walau pointi 3 ili aweze kubaki kundini.
Wananchi pia wanata pointi hizo tatu ili waweze kusonga kwenye hatua inayofuata kwenye michuano hii ambayo msimu uliopita walitolewa kwenye hatua za mapema kabisa chini ya Nabi.
Je msimu huu wanaweza kufika wapi huku wakiwa bado kwenye Ligi kuu ya NBC ndio wanaoongoza Ligi wakiwa mbele pointi 8?
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumamosi tarehe 26 siku ya Jumapili saa 1:00 usiku.