Yanga Yaikazia Simba Kumuaga Jonas Mkude

Klabu ya Yanga kupitia Afisa habari wao Ally Kamwe wamesema kuwa kama Simba wanataka kumuaga Jonas Mkude kwa mara ya mwisho waende kumuaga siku ya kilele cha wananchi.

 

Yanga Yaikazia Simba Kumuaga Jonas Mkude

Afisa habari huyo aliongeza kuwa wanawakaribisha Simba siku hiyo ambayo itafanyika Jumamosi Julai 22 mwaka huu na watawapa nafasi ya kumpigia “salute” na parade halafu watawaruhusu waondoke na wakaendelee na shughuli zao zingine.

Mkude yupo kwaajili ya Yanga n akuwapa furaha wanayanga, na ataonekana siku ya kilele cha wananchi pekee. Alisema Ally Kamwe.

Yanga Yaikazia Simba Kumuaga Jonas Mkude

Ikumbukwe kuwa Mkude ndiye aliyekuwa mchezaji mkongwe zaidi katika klabu ya Simba baada ya kutumikia kw amiaka 13 na hatimaye msimu huu klabu hiyo ya Msimbazi ikaamua kuachana naye.

Je kutokana na kauli ya afisa habari huyo wa Yanga, Simba ichukue uamuzi gani? imuage au iachane nayo?. Hayo yote yapo mikononi mwa Simba ambao kwasasa wapo Uturuki kujiandaa na msimu ujao.

 

 

Acha ujumbe