Klabu ya Yanga imeendelea ilipoishia siku ya Jumatatu dhidi ya Azam FC na leo imefanikiwa kuifunga klabu ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa ligi kuu ya NBC jioni ya leo.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa uulishuhudia klabu ya Yanga imefanikiwa kupata ushindi wa mabao mawili kwa bila mabao yaliyofungwa na Maxi Nzengeli.Mchezo huo ulionekana kutawaliwa zaidi na mabingwa hao watetezi wa ligi ya NBC tangu dakika ya kwanza ya mchezo, Japo Singida Fountain Gate walioneakana kutoa upinzani lakini mwishoni ni Wananchi walioibuka kinara.
Mchezo huo ulikua wenye ushindani mkubwa ambapo Wananchi walionekana kuendelea kuonesha ubora na ukubwa wao, Kwani licha ya Singida kuoneakana kupambana lakini hawakufua dafu na kushindwa kupata bao hata moja.Klabu ya Yanga wanaendelea kukaa juu ya msimamo wa ligi kuu ya NBC wakiwa na alama 18 wakiwa wamecheza michezo saba mpaka sasa, Huku wakifanikiwa kushinda michezo sita na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya klabu ya Ihefu Fc.