Yanga Yamaliza Mwaka Kileleni

Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kumaliza mwaka 2022 ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC kwa mara ya pili mfululizo ikirudia ilichokifanya mwaka 2021.

Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kupata alama tatu muhimu dhidi ya klabu ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliopigwa katika dimba la Manungu mkoani Morogoro, Bao pekee la klabu hiyo lililowapa alama tatu limefungwa na kiungo wa bei ghali Stefane Aziz Ki.yangaKlabu hiyo imefanikiwa kufikisha alama 50 baada ya kucheza michezo 19 hivo kuwafanya kuendelea kusalia katika kilele cha msimamo wa ligi kuu ya NBC, Na kufanikiwa kuwaacha mahasimu wao klabu ya Simba waliopo nafasi ya pili kwa alama sita kwani wao wana alama 44.

Wananchi ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC wamefanikiwa kumaliza kileleni kwenye kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya kumaliza kileleni mwaka 2021, Huku wakifanikiwa kua mabingwa na sasa wamemaliza kileleni inasubiriwa kama wataweza kutetea ubingwa wao.yangaTofauti ya Yanga iliomaliza kileleni mwaka 2021 na hii iliyomaliza mwaka 2022 ni kua mwaka jana klabu hiyo ilifunga mwaka kileleni, Lakini ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja mwaka huu tayari imeshapoteza mchezo mmoja dhidi ya Ihefu Fc kutoka Mbeya.

Acha ujumbe