WAKATI akiwa anatajwa kutaka kuondoka ndani ya kikosi cha Yanga mabosi wamemkomalia nyota wao mwenye mabao 24 katika mashindano ya Kombe la Shirikisho na Ligi Kuu Bara.
Ni Fiston Mayele mwenye mabao 17 kwenye ligi akiwa na mabao 7 kwenye Kombe la Shirikisho Afrika na kote kasepa na kiatu cha mfungaji bora nyota huyo wa kimataifa wa Congo.Nyota huyo mkataba wake umesalia mwaka mmoja ndani ya Yanga anatajwa kuwa kwenye hesabu za Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambayo inahitaji saini yake.
Ali Kamwe amesema kuwa watazugumza na Mayele ili kumpa nafasi ya kuendelea kula mema ya nchi katika ardhi ya Tanzania.
“Ambacho tunakifanya ni kuzungumza na Mayele ambaye ni mchezaji wa Yanga na kikubwa ni kutaka kuona kwamba anaendelea kula mema ya nchi.“Tutafanya maboresho kwenye mkataba wake na kuona namna gani ataendelea kuwa pamoja nasi lakini ikitokea kutakuwa na ofa kubwa zaidi hilo ni jambo ambalo litajadiliwa kwa manufaa ya pande zote,” amesema Kamwe