Yanga Yamuongezea Mkataba Gamondi

Klabu ya Yanga inaelezwa imekubaliana na kocha wake wasasa Miguel Gamondi na kumuongezea mkataba ambao utaendelea kumuweka kwenye mitaa ya Twiga na Jangwani.

Kocha Miguel Gamondi ambaye alisaini mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu ya Yanga na akiwa tayari ameutumikia mkataba huo, Mazungumzo yalikua yanaendelea baina yake na klabu hiyo mpaka pale ambapo ametambulishwa kwenye mkutano wa Wanachama wa klabu hiyo ikielezwa bado yupo sana.YangaIkumbukwe kocha huyo alitambulishwa kwenye mkutano mkuu wa wanachama wa mwaka mwaka jana na hata suala la yeye kuongeza mkataba wa kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo ya Wananchi limeonekana kutangazwa siku ileile ambayo ambayo alitangazwa kua kocha mkuu.

Haijafahamika kocha huyo ameongeza mkataba wa miaka mingapi vilevile haijawekwa wazi kua amesaini ila viashiria ambavyo vimeoneshwa kwenye mkutano huo mkuu wa wanachama ni wazi kua kocha huyo amesaini kandarasi mpya ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa msimu mwingine.YangaMpaka sasa mtihani ambao unaonekana kubaki kwa klabu ya Yanga baada ya kumpa mkataba kocha wao Miguel Gamondi ni kumbakiza staa wao klabuni hapo Stephane Aziz Ki ambaye amemaliza mkataba wa kuitumikia timu hiyo, Hivo hiyo ni kazi nzito ambayo inawakabili viongozi wa klabu hiyo.

Acha ujumbe